Advertisements

Sunday, August 14, 2016

MWANAMKE NI PAMBO LA DUNIA ACHA KUMNYANYASA - MAGANGA ONE

Ewee ndugu yangu mwanaume,Je unafahamu kama wanawake waliumbwa hapa duniani ili kuipamba hii dunia? Hakuna mwanaume ambaye hajui hili na kama kuna mwanaume ambaye hafahamu uwepo wa mwanamke kwenye hii dunia kuwa ni pambo basi leo nitajaribu kuwakumbusha wengi wa wanaume wenzangu ambao hawafahamu uwepo wa bustani zetu hizi.

Kuna baadhi ya wanaume kwao imekuwa kama itikadi au mila kwa kuwanyanyasa,kuwatukana na hata kuwapiga wanawake zao majumbani.Mwanamke hakuumbwa kupata aina yoyote ya msukosuko hapa duniani,mwanamke kaumbwa awe pambo la hii dunia na kama wanaume tunahitaji uelewa wa kutunza bustani zetu hizi ili kuleta uzuri uvutiao duniani.

Kila bustani inahitaji matunzo sana ili ipendeze,kama mwanaume muhudumie sana mkeo na kumpenda ili aonekana vyema na mwenye nuru kila kukicha.Msongo wowote wa mawazo umpeleke mwanamke kudhohofu kiakili na hata taswira ya uso wake na hapo ndipo kila mmoja uhisi kwamba huyu mwanamke ana tatizo.Kwanini uwape watu hisia tofauti juu ya mkeo au msichana wako?

Wengi wa wanaume wamekuwa na lugha mbaya sana majumbani pindi wakijua wao ndio tegemezi kwa wanawake wao..Wanasahau kuwa huduma wanazozitoa kwa wanawake zao ni wajibu wao na sio hiari kwao.Yale maneno mabaya wanapoyatoa kwa wake zao wanajisahau kwamba mwanamke ni mtu ambaye kajaaliwa uwezo wa kusamehe ila kusahu huwa hasahau kamwe,tukio lolote la unyanyasaji uleta athari sana ndani ya nafsi tena haswa kwa kina mama.Wanaume wengi wamekuwa na tabia ya kujitoa fahamu kwa kusema eti "sijali" Hujali vipi na wakati kipindi kile unatoa maneno yako mazuri ili aje awe mkeo nyumbani leo hii unaposema hujali unakuwa na maana gani hasa?Usiharibu sifa ya wanaume wenzako kwa kuharibia taratibu na sifa nzuri ambazo mwanaume anahitajika kuwa nazo.

Mwanaume mmoja anaweza kuchafua jina la wanaume wengine bila kujua kwa kuwa anafanya matendo ambayo hayaipendezi jamii ya jinsia ya upande wa pili{kina mama}.Mwanamke mmoja akitendwa na mwanaume na akayapata maumivu haswaa huwa ana nguvu ya kuwashawishi wanawake wenziwe kuwachukia wanaume wengine na ikawezekana bila shaka.Wanaume tuachane kabisa na tabia za kuwadharau wake zetu,kuwanyanyasa wake zetu,kuwatukana na hata kuwapiga.Kuna njia nyingi mbadala za kuwakanya kina mama ili kuendana nao vizuri majumbani mwetu tunapoishi.kumbuka kumpiga mwanamke sio suluhu ya mapenzi ndani ya nyumba,kumtukana mwanamake ni ukosefu wa adabu ambao unajivunjia hata wewe mwenyewe mtukanaji bila kujua.Kitendo cha kumnyanyasa mwanamke sio haki kabisa kwani ulimtoa kwao kwa taratibu nzuri na kutokana na lugha au utaratibu mzuri mliotumia ili wazee wake wakubaliane nanyi na ndipo uliaminika kwamba utakwenda kumtunza mtoto wa watu vyema,kinyume cha hayo ni kwamba unaonyesha udhaifu ambao sio sifa ya wanaume.Jirekebisheni wanaume juu ya suala zima la kuwatunza na kuwapenda wake zenu..

Leo niishie hapa na naomba liwe somo kwa wanaume wenzngu,kwa kila atakayesoma tafadhali amsukumie ujumbe huu mwenzake na mwenzake ili liwe somo kwa jamii inayotuzunguka.

Makala hii fupi imeandikwa na Maganga One Blogger

Nakaribisha maswali na maoni kupitia email yangu ya magangaone@gmail.com na simu yangu +32 466 47 05 92

Unaweza kunifuatilia kwa Instagram yangu ya maganga_one

Facebook page yangu maganga one blog na what'sapp kwa namba yangu hiyo hapo juu.Shukrani kwa wasomaji wangu wote wa Maganga One Blog.

No comments: