Advertisements

Saturday, August 13, 2016

SHUKURANI WANADMV

Wapendwa ndugu zangu wana DMV (District of Columbia, Maryland na Virginia) na
ndugu watanzania kutoka states mbalimbali, Salaam. Kwa niaba ya familia yangu na
kwa niaba yangu binafsi napenda kutoa shukrani zangu kwa mtiririko wa ajabu na wa
upendo ambao ulikuja kwetu tangu tulipofikwa na msiba mzito huko kijiji cha Sima,
wilayani Sengerema, mkoa wa Mwanza, Tanzania mwezi May 11, 2016. Natoa shukrani
kwa faraja mliyo tupa wakati wa kipindi cha majaribu. Binadamu huwa tuna umia sana
kupoteza wapendwa wetu hata tunapoona wanaumwa kupindukia na kwa muda mrefu.
Lakini msiba huu ulikuwa tofauti. Mlitufariji mno.

Tuna shukuru sana kwa michango mingi ambayo ilitolewa kwa upendo ili kufanikisha
mazishi. Kwa niaba ya familia, ninatoa shukrani za kina kwa ukarimu wenu mlio
uonyesha kutoka ndani ya mioyo yenu. Naishukuru serikali ya Tanzania, hususani
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu kwa kufika nyumbani, pia na serikali ya mkoa na
wilaya kwa msaada uliotolewa.

August 6, 2016 kulifanyika misa kumshukuru Mungu na kuwakumbuka waliotuacha,
kama Mtume Paulo alivyosema: Mshukuru Mungu kwa kila jambo; (Wathesalonike
5:18). Hata ikiwa ni nyakati bora au nyakati mbaya, Mungu yupo pamoja nasi.
Wapendwa wengi wanaoishi DMV na majimbo mengine ya USA jumla ya watu karibu
mia tatu walihudhuria.

Inakuwa vigumu sana kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja kutokana na ushirikiano
wenu mlio utoa. Sina maneno ya kutosheleza shukrani zangu kwenu, maana najua
maneno peke yake hayatoshelezi na hayawezi kuonyesha faraja kubwa niliyo nayo mimi
na familia yangu kutokana na upendo wenu mliouonyesha.

Napenda pia kushukuru ofisi ya Ubalozi wetu wa Tanzania hapa Washington D.C. kwa
uwakilishi wenu; Ndugu Colonel Aldolph Mutta na ujumbe wake walikuwako. Kutokana na muda
kuwa mdogo hamukuweza kupata nafasi kutoa salaam lakini, uwakilishi wenu
haukupita bila kutambulikana. Mbarikiwe sana.

Napenda pia niishukuru ofisi kuu ya Evangelical Lutheran Church in America (ELCA): Africa Desk kwa kukubali kutupatia Mhubiri Mch. Nicholaus Chove kutoka Texas. Alifanya kazi nzuri sana, na Mungu asifiwe sana.

Kwa kumalizia napenda tena kusema asanteni sana kwa kufika kwenu kwenye ibada.
Napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwa akina mama waliojitolea kwa moyo
mkunjufu kututayarishia chakula, Nawashukuru akina baba kwa kuleta vinywaji laini.
Nawapenda na Mungu awabariki sana.

Mch. John Mbatta

No comments: