ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 6, 2016

TAASISI YA VIJANA YA TYVA YAADHIMISHA MIAKA 16 YA KUUNDWA KWAKE

Katibu tawala wa Manispaa ya  Ilala, Mh.Edward Mpogolo(wa pili kutoka Kulia) akikata keki na Mwenyekiti wa TYVA, Nuria Mshare wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya taasisi ya Vijana ya TYVA  iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council. wa kwanza kulia ni Afisa vijana wa Jiji la Dar es Salaam, Masalida Zephania Njashi na wa kwanza kutoka kushoto ni Zulekha Ibrahim. (Picha na Geofrey Adroph)
Pia mgeni rasmi alizindua kitabu cha mtazamo wa Vijana Bajeti ya mwaka wa fedha ya 2016/2017 kilichoandikwa na Taasisi la Vijana la TYVA pamoja na kuzindua Dokumentari ya Video ya Binti Jitambue.

Katibu tawala wa Manispaa ya  Ilala, Mh. Edward Mpogolo akuzungumza na vijana wa shirika lisilo la kiserikali la TYVA waliofika katika maadhimisho ya miaka 16 ya shirika hilokatika ukumbi wa British Council leo jijini Dar.
Katibu Mtendaji wa   TYVA Saddam Khalfan akieleza mafanikio pamoja na changamoto walizozipata ndani ya miaka 16 ya taasisi ya vijana ya TYVA pia alizingumzia masuala ya Ajira kwa Vijana, Uhamasishaji wa ulipaji wa Kodi pamoja na masuala ya Bajeti  na Katiba kwa vijana iliyofanyika leo katika ukumbi wa British Council jijini Dar.
 Afisa vijana wa Jiji la Dar es Salaam, Masalida Zephania Njashi akizungumza na vijana waliofika katika maadhimisho ya miaka 16 ya taasisi ya Vijana ya TYVAyaliyofanyika katika ukumbi wa British Council leo jijini Dar

Aliyekuwa Mwananchama  wa TYVA  Costantine Deus akieleza mafanikio waliyoyapata ndani ya kipindi cha miaka 16 wakati wa maadhimisho yaliyofanyika leo jijini Dar.
Mkuu wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka  Taasisi ya Vijana ya TYVA ,Suleiman Makwita akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya  taasisi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa British Council leo jijini Dar.
   Baadhi ya vijana waliofika katika maadhimisho ya miaka 16ya taasisi ya Vijana ya TYVA

Emmy Leonard akitoa ushuhuda kuhusu taasisi ya Vijana ya TYVA alivyomsaidia mpaka kuwa mjasiliamali 
 Baadhi ya wadau pamoja na vijana waliofika katika maadhimisho ya miaka 16 ya taasisi ya vijana ya TYVA iliyofanyika katika ukumbi wa British Council leo jijini Dar.

No comments: