Advertisements

Sunday, August 14, 2016

TANZIA ABOUD JUMBE AFARIKI DUNIA

Rais wa zamani wa Zanzibar, marehemu Aboud
Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia leo saa 7.00 mchana Mjimwema, Kigamboni jijiji Dar es Salaam.

Mtoto wa Marehemu, Mustafa Aboud Jumbe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kwamba atazikwa Zanzibar kesho saa 7.00 mchana.

“Ni kweli mzee Jumbe amefariki leo nyumbani kwake Kigamboni mbele ya familia yake na atazikwa kesho Zanzibar,” amesema.

Kwa taarifa zaidi soma gazeti la Mwananchi kesho au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz

No comments: