Advertisements

Saturday, August 13, 2016

TGNP YAKUTANA NA WAHARIRI KUJADILI UTAFITI WA URAGABISHI NA BAJETI YA MWAKA 2016/17 KATIKA MLENGO WAKIJINSIA

 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TGNP Mtandao, Dk. Alexander Makulilo akifungua majadiliano kwa wahariri wa vyombo vya habari kuhusu utafiti wa uraghabishi na Bajeti ya mwaka 2016/17 yaliyoandaliwa na Shirika la TGNP Mtandao.


 Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao, Lilian Liundi akiwafunda baadhi ya wahariri kuhusu umuhimu wa uraghabishi katika mkutano wa majadiliano uliofanyika leo.
Afisa Program uchambuzi na Machapisho kutoka TGNP Mtandao, Bw. Deogratius Temba akitoa mada ya bajeti kwa mlengo wa kijinsia ya mwaka 2016/17 kwa baadhi ya wahariri waliofika katika majadiliano kuhusu uragabishi ambao umekuwa ukifanywa na Mtandao wa kijinsia Tanzania  wa TGNP.
Mzalishaji wa Vipindi kutoka TV1, Lulu A. Sanga akichangia mada 
Mhariri wa EATV, Rwehabura Rugambwa akichangia mada iliyokuwa ikuwa ikijadiliwa na wahariri pamoja na TGNP Mtandao
 Mhariri Mkuu wa Mlimani Tv, Amini Anthon Mgheni akichangia mada wakati wa majadiliano.

 Mkurugenzi Mtendaji TGNP Mtandao, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwahusisha wahariri katika majadiliano  yaliyokuwa yanahusu utafiti wa kiragabishi ambayo yamekuwa ukifanywa na Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP.

Na Mwandishi Wetu
IMESEMEKANA kuwa kupitia utafiti wa kiragabishi ambao umekuwa ukifanywa na Mtandao wa kijinsia Tanzania TGNP, wananchi wamehamasika kushirikiana na viongozi katika shughuli za maendeleo.
Hayo yalibainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji TGNP, Lilian Liundi katika warsha ya kutoa ulewa kwa Wahariri kuhusu bajeti ya mlengo wa kijinsi.
Alisema uragabishi pia unaboresha uchambuzi wa sera miongoni mwa wananchi hasa katika kuweka mipango madhubuti ya kwenye miradi ya maendeleo ya kianzaia ngazi ya kijiji hadi kitaifa.
“Kwa sasa sehemu ambapo utafiti huu umefanyika na kupata elimu namba ya watu kuudhuria mukitano ya kisera imeongezea na sio kuongezeka tu bali wanatoa maoni ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye maamuzi.
“Na sisi kama TGNP kitu hicho ndicho tunakitaka, kwamba wananchi washirikiane na viongozi wao kuleta maendeleo yaani vipaumbele vitoke kwa wananchi wenyewe, hayo ndiyo maendeleo,” alisema Lilian.
Akizungumzia ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za maamuzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk. Alexnda Makalilo, alisema bado kuna pengo kubwa kati ya wanaume na wanawake kwenye uongozi.
“Licha ya kwamba wanawake ni zaidi ya asilimia 50 na ndio wategemezi wakubwa kwenye suala la uzalishaji lakini idadi ya nafasi zao katika maamuzi ni ndgogo.
“Katika demokrasia tunesema kuwa walio wengi ndio huwa wanaamua lakini kwenye maamuzi wanaume ndio wanaamua, hapo kuna demokrasia kweli?,”alisema Dk.Makalilo.
Aidha Dk. Makalilo alishauri kuwekwa mikakati ya kuwaunganisha wanawake kuwa nguvu ya pamoja katika harakati za kutafuta usawa wa kijinsia. 

No comments: