Advertisements

Sunday, August 14, 2016

UKAWA YAKUMBUKA MITIKISIKO ILIYOPITIA WAKATI WA UCHAGUZI

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema uchaguzi wa mwaka jana haukuwa rahisi kwani Ukawa ilipitia katika mitikisiko mitatu.

Mtikisiko wa kwanza ni mchakato wa kumpata mgombea urais wa Ukawa ambao haukuwa rahisi kutokana na hali halisi ya uchaguzi huo, mtikisiko wa kuondoka kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na mwisho ni kutangazwa kwa matokeo ya urais.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi mwishoni mwa wiki, Mrema amesema mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Ukawa ulikuwa mgumu kutokana na mazingira yalivyokuwa kwa sababu vyama vya Chadema na CUF, kila kimoja kilikuwa na uwezo kutoa mgombea wa urais.

“Ninakumbuka mara kadhaa tuliwaita waandishi wa habari ili tumtangaze, lakini tuliahirisha kutokana na ugumu uliokuwapo katika mchakato huo,” amesema.

Mrema ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ndogo ya kuandaa mapokezi ya kumkaribisha, Edward Lowassa aliyetoka CCM.

Lowassa alijiengua CCM na kujiunga na Chadema siku chache baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kuwania urais mkoani Dodoma.

Mapema kabla ya jina lake kukatwa, Lowassa alikaririwa akisema hakuna wa kumkata jina lake, na kama akikatwa, kwanini akatwe wakati katika mapambano hakuwahi kushindwa.

Mrema amesema, kabla ya mchakato huo wa kumpata mgombea urais haujatulia, Ukawa ikapata mtikisiko wa kuchomoka kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Lipumba na baadaye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa.
MWANANCHI

1 comment:

Anonymous said...

Mtikisiko wa kujitakia kutokana na chadema kula matapishi yao mchana kweupe kwa kitendo chao cha kumpitisha Edward Lowasa kuwa mgombea wao kwa nafasi ya uraisi. Hata kupitishwa kwake katika nafasi hiyo hakupitishwa katika misingi ya kidemokrasia. Si hivyo tu muheshimiwa Lowasa, almaarufu "FISSADI" asingepata wasifa huo wa ufisadi kama si jitahada za chadema kumtangaza nchi nzima na nje ya Tanzania kuwa Edward Lowasa ni fisadi na muhujumu uchumi nambari moja. Kwa Lowasa siku zote, yeye kwanza nchi au chama baadae mtu wa aina hiyo ni hatari hata katika familia na hawezi kuhamia sehemu halafu hiyo sehemu ikabaki salama. Kulikuwa hakuna sababu ya Lowasa kuhama CCM kwa sababu ya kukosa nafasi ya kugombea uraisi. Mali zake zote,maisha yake na umaarufu wake wote hata huo wa ufisadi kaupatia CCM sasa kitendo cha Lowasa kuisusa CCM kwa sababu ya kukosa nafasi ya kugombea uraisi, kilimfichua Lowasa katika hali halisi ya ubinafsi alionao. Tukija katika masuala ya siasa kwa watanzania wanaofuatilia uchaguzi wa Marekani watagundua yakwamba kiongozi au mgombea ni vigumu kuwa zaidi ya chama na kama mtu huyo ataruhusiwa kuwa zaidi ya chama kuna uwezekano wa kiongozi huyo kuwa zaidi ya serikali. Kiuhalisia Bernie Sanders wa Democrat alikubalika zaidi katika kura za mtu mmoja mmoja,lakini Hillary Clinton ni dhahiri ni chaguo la chama na kwa kiasi fulani mpaka baadhi ya viongozi wa juu chama cha Democrats kama vile mwenyekiti wa taifa wa chama hicho kulazimika kujiuzulu kutokana na kashifa iliyovuja yakwamba walishakuwa wamemuekea Hillary Clinton mazingira mazuri yakuwa mgombea wa uraisi kupitia chama hicho na ni kweli Hillary ni mgombea wa uraisi wa chama hicho hivi sasa. Bernie Sanders aliekuwa mpinzani wa Hillary Clinton kalalamika na kulaani na kulani vikali kwa yote aliyoyaona na kuyasikia kuhusu yakuwa alikuwa akijahangaisha bure lakini vigogo wa chama tayari walishakuwa na mtu wao. Hatua gani Bernie Sanders alichukuwa baada ya kugundua kuhujumiwa katika mbio zake za kuwania uraisi? Baada ya hali hiyo kutokea kwa Bernie Sanders ameamua kujikita zaidi ndani ya chama na kuhakikisha siku za usoni chama kinampata mgombea wake kwa njia ya haki zaidi.Bernie Sanders alikuwa anakubalika na wamerekani wengi hata wale wa upande wa upizani yaani republicans mara nyingi tu kuliko Edward Lowasa alivyokuwa anakubalika katika uchaguzi wa Tanzania uliopita lakini hakupitishwa na chama chake na hakikusia chama chake au kuhama ni mzalendo wa kweli wa chama na hakuendekeza ubinafsi yakuwa yeye kwanza chama baadae kama viongozi wengi hovyo wa kiafrika. Nasema chama ndicho kilicho mteua Hillary kwa sababu katika siasa za Marekani kura za mbunge na wabunge maalum katika chaguzi za ndani ya chama huwa zinanguvu mara zaidi na zaidi kuliko kura ya raia au mwanachama wa kawaida na hao ndio waliomchagua Hillary. Sasa laana ya Lowasa ndani ya chadema itawatafuna sana na mitikisiko zaidi inakuja mbele yao mpaka wakamuangukie Dk Slaa. Ndipo chadema itakapo jirudi upya.