Dar es Salaam. Utekelezaji wa dhamira ya Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda kuuchenjua nje ya nchi akitaka shughuli hizo zifanyike nchini, umeelezwa kuwa utachukua muda mrefu kutokana na mchakato wake.
Juzi, Rais Magufuli alinukuliwa na vyombo vya habari wilayani Kahama akisema katika uongozi wake hataki kuona mchanga huo ukisafirishwa.
Agizo hilo limekuja wakati utafiti juu ya uwezekano wa Tanzania kuwekeza katika mtambo wa kuchenjua mchanga wa dhahabu ya uliofanywa na Wakala wa Ukaguzi Madini Tanzania (TMAA) Februari 2011, ukionyesha kuwa ni uwekezaji unaohitaji fedha nyingi.
Ripoti hiyo imesema gharama za usimikaji mtambo kamili wenye uwezo wa kuchenjua wastani wa tani 150,000 kwa mwaka, ingeweza kufikia Dola za Marekani 500 milioni hadi Dola 800 milioni (sawa na Sh1.1 trilioni hadi Sh1.74 trilioni za sasa).
No comments:
Post a Comment