Advertisements

Wednesday, August 3, 2016

VYUO 175 NCHINI VYAPEWA NOTISI YA KUSHUSHWA HADHI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mhandisi Steven Mlote(kushoto)akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,wakati wa kutoa tamko la baraza hilo kuvifutia Usajili baadhi ya vyuo na vyuo 175 vimepewa notisi ya kushushwa hadhi,5 vyafutiwa Usajili na 41 vimetakiwa kujisajili mara moja,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,ikiwa katika jitihada za kuboresha elimu ya ufundi nchini,Katikati Kaimu wa baraza hilo Dkt. Adolf Rutayuga na Mkurugenzi wa Udhibiti,Ufuatiliaji na Tathimini Bi. Agness Ponera

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limetangaza kuwa vyuo 5 vimefungwa kuendesha mafunzo na kufutwa kwenye rejista ya vyuo vya ufundi nchini.
Pia Baraza limetangaza kuwa vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria vimepewa muda wa wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Vilevile, vibali vya usajili wa vyuo 112 vya kutoa elimu ya ufundi vimefikia ukomo hivyo vinapaswa kutekeleza masharti ya Usajili; wakati vyuo 57 vimefikia ukomo wa ithibati, hivyo inapaswa kutekeleza masharti ya ithibati, imetangazwa jana.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza (NACTE), Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.


Mhandisi Mlote pia alitoa onyo akisema “vyuo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria nimevipa muda wa wiki mbili na navitaka vijisajili mara moja kwenye Baraza kabla ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria”.

Mhandisi Mlote alivitaja vyuo vyote vyenye matatizo kama ifuatavyo:










No comments: