Wakati viongozi wa dini wakiendelea na jitihanda za kusaka suluhu kati ya upande wa Serikali na Chadema kuhusu namna ya kuzuia kwa amani kufanyika kwa Operesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, Septemba 1, Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametoa maoni yake.
Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa haoni haja ya kufanyika kwa vikao hivyo vya kusaka maridhiano kwani Chadema wanachotaka kufanya kiko kikatiba.
“Sioni ni kwanini tunahangaika na vikao vya maridhiano na tahariri nyingi kuhusu shughuli ya CHADEMA kufanya operesheni yao ya UKUTA. Kuandamana ni Haki ya KIKATIBA. Tuache watu watimize Haki yao Kwa amani. Kuzuia watu kufanya jambo lao la kikatiba ndio kuvunja amani. Wanaotaka kuandamana waandamane na wanaotaka kufanya Kazi zao nyingine tuendelee na Kazi zetu. Kwanini kutekeleza Haki ya kikatiba iwe ni kuvunja amani? Kwanini?,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Hata hivyo, vikao vya maridhiano vinavyoendelea tayari vimeonesha kuzaa matunda kwenye suala la mgogoro wa Bunge ambapo wabunge wa vyama vya upinzani wameridhia kurejea Bungeni katika vikao vitakavyoanza mapema mwezi ujao.
Serikali imeendelea kuwaonya watu wote wanaopanga kuandamana Septemba 1 huku viongozi wa Chadema wakisisitiza kuwa siku hiyo watafanya maandamano kama walivyopanga.
Hali hiyo imepelekea kumtoa hadharani Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ameomba marais wastaafu kumshauri Rais Magufuli ili kuruhusu Serikali kukaa na Chadema kusaka muafaka wa masuala ya kisiasa nchini.
4 comments:
Huo ndio ukweli na Tanzania bado ni nchi ya vyama vingi. Waliopewa madharaka wanaiminya haki hii ya kikatiba kwa makusudi na huu ndio uoga ambao haukubaliki, Viongozi waliopita waliifuata katiba na hakukuwa na polisi kuingia barabarani kwa mazoei kama vile tuko vitani.
Haki inapominywa je unategemea amani iwepo? Wanatafuta njia za mkato sivyo siasa inavyoenda.
Wote, Zito Kabwe na ndugu zake wa ukawa na kadhalika ni watu wa hovyo. Nguvu kubwa zinatumika kwa upande wa upizani kumpiga vita Magufuli kwa kisingizio cha demokrasia wakati ni kwamba Maghufuli anaijenga nchi katika masuala ya msingi yanayoikabili nchi yetu hasa umasikini uliosababishwa na uzembe na ufisadi uliojengeka katika maisha ya kila siku ya mtanzania. Yaani kweli tunakubali kuwasikiliza akina Mbowe watu ambao lengo lao kubwa ni kushika madaraka kwa tamaa zao binafsi kwa kisingizio cha demokrasia na kuanza kumbeza Magufuli mtu ambae kwa hata mataifa ya wenzetu yanatushangaa kuacha kumpa kila aina ya sapoti kulisukuma taifa letu mbele kimaendeleo. Kweli watanzania twenye akili zetu tukubali kuacha kumuunga mkono muheshimiwa raisi kwa yale anayoyafanya sasa kwa kuwasikiliza watu ambao wana mipango hewa ya maendeleo na ahadi feki za demokrasia kwani China kuna vyama vingi na maandamano? Kinachotakikana ni maendeleo Bana! Hizo nchi zote zinazojifanya za kidemokrasia kiuhalisia waneshafika pabaya. Waneanza na hoja ya watu wawe na uhuru wa kusema hata kama wakimtukana Mungu ok sawa. Wakaja tena wanawake wawe na haki sawa na wanaume at least it does make sense, okay sawa.wakaja tena ah wanawake wawe wanakwenda uchi hadharani kama wanyama ndio wanapendeza zaidi okay sawa. Hawajatosheka ah mbwa anahuruma zaidi ya mwanadamu hasa mwanadamu wa kiume kwa hivyo ni bora akawa na haki zaidi kuliko mtu wa kiume katika familia na ndio maana wala sio chumvi kwa huku ulaya au Marekani haki ya msingi katika familia inaanzia kwa mtoto halafu anfuatia mwanamke halafu tena anafuatia mbwa kama familia inamiliki mbwa halafu mtu wa mwisho ndio anafuatia mwanamme. Na hilo nalo okay sawa demokrasia,ukimkuta mbwa kalala ubavu mmoja na mkeo huna ruhusa ya kumwamsha uwende ukalale kwenye sofa. Hee! Hawaja tosheka maana huu mkwara wao wa demokrasia unafanya kazi umewapa kiburi kujifanya Waungu watu wa kuwapangia watu wa mataifa mengine jinsi ya kuishi au hampati misaada na vijinchi maskikini vya kiafrika vilikuwa vinafanya vizuri katika mfumo wa chama kimoja kwa tamaa ya kugaiwa misaada vikaingia kwenye vyama vingi na baada ya hapo ndio ikawa mwisho wa pride of Africa imebakia jina tu. Somali ilikuwa nchi nzuri kuliko nchi nyingi za kiafrika utaniambia wewe mdau iko wapi Somali hivi fitina imefanya kazi yake? Zimbabwe ikijulikana almaarufu kama Beacon of Africa kutokana na kunona kwa maendeleo kwa kumtumia Changarawe mtu wa upizani wa Mugabe, haipo tena ile Zimbabwe huo usemi wa kusema aah Mugabe dikteta. Dikteta hachukui ardhi ya nchi zima iliokuwa imemilikiwa na asilimia tano ya watu na kuwagia wananchi waliowengi. Hata vijinchi kama Zambia vilikuwa vikifanya vizuri zaidi wakati huo chini ya demokrasia ya chama kimoja. Sasa utaona hiyo hulka ya demokrasia kutoka nchi za kibepari inavyo walevya na kumkebehi hata Mungu sasa deal of the town ni Usenge au ushoga uwe wa kike au kiume yaani sasa katika familia za nchi za ng'ambo au ughaibuni Msenge au Shoga kachukua nafasi ya kwanza katika familia kumshinda hata mtoto kwa haki za msingi. Kuwa na msenge katika familia za wenzetu ni deal na mtandao wao una nguvu za kila aina.pesa,ajira,yaani opportunity kede wa kede kiasi kwamba kimewavutia watu wengi hasa vijana kuona kuwa ni kitu cha maana sana na kama umebahatika kupita pita katika viunga vya New York city basi utafahamu nini tunachokiongea kuhusiana na suala la ushoga na hiyo yote ni matunda ya demokrasia na sasa kuna nguvu kubwa zinatumika hivi sasa kuhakikisha waafrica wanakamilisha demokrasia kwa kuiridhia sera ya usenge.kwa hivyo wanaofoka na kujiapiza lazima waandamane kwa kuwa ndio demokrasia kwa kweli sio kila kitu kinachoitwa demokrasia kitakuwa na manufaa katika jamii na inawezekana kabisa kuwa ni chanzo cha maafa na tunatakiwa kuwa waangalifu tunapojaribu kuigiza kitu cha mtu, lakini kama tunamzungumzia baba wa Maendeleo hivi sasa duniani ni Mchina tutake tusitake na jee wachina wamefika pale walipo sasa kwa blah blah ya maandamano au uchapaji wa kazi?
Nilikuwa supporter mkubwa sana wa Rais Magufuli na CCM wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana. Lakini nimekuwa disappointed sana na utendaji wa kazi wa Rais Magufuli. Anakandamiza demokrasia na anatawala kimabavu. Dhana ya uongozi wa utawala bora haielewi. Anadhani kuwa Rais ni kuwa mfalme katika absolute monarchy kama Saudi Arabia. Ni kweli Watanzania tunataka maendeleo lakini tunataka uhuru vilevile. Zamani alikuwa anaitwa jembe na bulldozer kutokana na sifa yake ya uchapakazi lakini nickname yake mpya ya Dictator nayo inamstahili kutokana na jinsi anavyotawala kibabe. Mungu isaidie Tanzania.
Nenda kalale wewe kama umelipwa sema ..usituletee story za panya na paka
Post a Comment