ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 28, 2016

BAADA YA TIMU YA SIMBA SC KUSEMA WANAANZA UJENZI WA TIMU YAO NAO YANGA FC WAJA NA HII JITIRIRISHE.

MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari zaidi ya 700 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay, Sizya Lyimo Kaimu katibu mkuu Baraka Deusdedit.

Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa kijiji cha michezo cha yanga ambapo patakuwa na uwanja wa kisasa wa mazoezi pamoja na wa mechi pia patakuwa na hosteli kwaajili ya wachezaji patakuwa na Hospital na shule.
MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lilipo Geza Ulole, Kigamboni, Dar es Salaam.Wasaidizi wa Manji wamekabidhi eneo hilo leo mchana katika hafla fupi iliyohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Maofisa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Aliyepokea eneo hilo kwa niaba ya klabu ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu, Mama Fatma Karume aliyeambatana na Mjumbe mwingine wa Bodi hiyo, Dk. Jabir Idris Katundu, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, Samuel Lukumay na Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit.

Sasa rasmi utafanyika ujenzi wa uwanja na uwekezaji mwingine katika eneo hilo lililobatizwa kijiji cha Yanga SC.
Ujenzi utakapokamilika, Yanga itakuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unatarajia kuwekewa nyasi bandia.

Baada ya kukabidhiwa Mama Karume alisema: “Nilizungumza na Manji, nikamuambia  kuendelea kufikiria Kaunda ni kujidanganya. Wenzetu Simba wanakwenda Bunju, sisi twende Kigamboni. Unajua maana ya Geza Ulole ni Jaribu Uone, tukiwa na uwanja huku, kila atakayejaribu kuja tutamfunga,”alisema na kupata makofi ya pongezi.


1 comment:

Anonymous said...

Kiswahili gongana,ameipa kivipi wakati Yanga kwa sasa ni Mali yake kwa miaka 10,sema kajipa mwenyewe