Advertisements

Friday, September 2, 2016

CGP - JOHN MINJA AMVISHA CHEO CHA KAMISHNA MSAIDIZI AFISA MWANDAMIZI WA MAGEREZA


Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matani ambaye alikuwa Nchini Namibia kwa jukumu la kuandaa Pogramu za Mafunzo ya Uendeshaji wa Magereza wa nchi hiyo kwa muda wa miaka miwili mfululizo. Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 3, 2016 Makao Makuu ya Magereza, Jijini Dar es Salaam.
Makamishna wa Magereza wakifuatilia zoezi la uvishaji cheo hicho kwa Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matanicha ambaye alikuwa Nchini Namibia kwa jukumu la kuandaa Pogramu za Mafunzo ya Uendeshaji wa Magereza wa nchi hiyo(kushoto) ni Kamishna wa Utawala na Fedha, Gaston Sanga(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akimvisha Kofia ya cheo cha Kamishna Msaidizi wa Magereza, Afisa Mwandamizi wa Magereza, Gideon Matani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Magereza baada ya zoezi la uvishaji Cheo kwa Kamishna Msaidizi wa Magereza, Gideon Matani(Picha zote na Lucas Mboje wa Magereza).

No comments: