Advertisements

Monday, September 26, 2016

CSI watoa mafunzo kwa Wakunga kutoka katika Hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Childbirth Survival International(CSI) akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya wakunga yaliyofanyika kwa takribani wiki mbili na kuwakutanisha wakumga mbalimbali kutoka katika hispitali za jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo alisema wakunga wakiendelea kupewa mafunzo ya kutosha wanaweza kuwasaidia kuokoa vifo vya mama na mtoto hiyo yote ni kwasababu amekutana na mkunga mwenye stadi za kutosha.
Muhitimu wa mafunzo ya ukunga akisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa kufunga kwa mafunzo hayo yaliyodumu kwa  wiki mbili yaliyofanyika katika chuo kikuu cha St. John kampasi ya Dar es Saalam.

Diwani wa kata ya Ukonga, Juma Mwapopo akitoa neno kwa wahitu waliomaliza mafunzo yaliyotolewa na CSI ili kuwaongezea ujuzi wakunga watakapo kuwa kazini.
Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Sued Kafano akitoa neno wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo kwa wakunga yaliyokuwa yananendehwa naCSI
Baadhi ya washiriki wakikabidhiwa vyeti uya kuitimu mafunzo hayo yaliyofanyika katikachuo kikuu cha S. John kampasi ya jijini Dar
Mkurugenzi wa Kays Hygiene Produts Limited, Khadija Simba akizungumza jambo baada ya kutoa zawadi kwa wakunga washiriki walioshiriki mafunzo ya wiki mbili ili kujiongezea ujuzi,
Picha ya pamoja

No comments: