Advertisements

Friday, September 16, 2016

HUKUMU YA KUMLAWITI MWANAE YAMFANYA AJIUWE KWA KUNYWA SUMUBy Waandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Moshi/Hai. Hassan Mtiko (49) amejiua kwa kunywa sumu, muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela kutokana na kupatikana na hatia ya kumbaka na kumlawiti mwanaye mwenye umri wa miaka 11.

Tukio hilo lililotokea juzi mchana eneo la Bomang’ombe mjini Hai, limezua gumzo maeneo mbalimbali ya mji huo.

Mfungwa huyoalikunywa sumu akiwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Bomang’ombe wilayani Hai, muda mfupi baada ya kuwaomba ruhusa askari kwenda chooni kujisaidia.

Chanzo cha habari kilieleza kuwa baada ya kuhukumiwa adhabu hiyo, mfungwa huyo alipelekwa mahabusu ya polisi akisubiri kupelekwa gerezani.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mahabusu walianza kumuona akiugulia maumivu na kutoa taarifa kwa askari mahakamani hapo.

Baada ya kunywa sumu hiyo juzi mchana, mfungwa huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Hai na kufariki dunia jana mchana.

No comments: