Advertisements

Tuesday, September 20, 2016

KORTINI KWA KUIDHALILISHA POLISI KWA WHATSAPP

Zikiwa zimepita siku tano tangu wakazi watano wa Dar es Salaam walipopandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Kisutu kwa kosa la kumdhalilisha Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi kwa kutumia mitandao ya Facebook na Whatsapp, mkazi mwingine ameongezeka.
Jana, mfanyabiashara Christon Mbalamula (28), alifikishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kutumia mtandao wa Whatsapp kwa kulidhalilisha jeshi hilo.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk Yohana Yongolo, Wakili wa Serikali Winifrida Sumawe alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 26, 2016 eneo la Kigamboni.
Alidai siku ya tukio, mshtakiwa huyo alilidhalilisha Jeshi la Polisi baada ya kusambaza ujumbe uliosema, “Natangaza ndoa na askari yeyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.” Baada ya kusomewa shtaka hilo alikana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi haujakamilika.
Hakimu alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kila mmoja asaini bondi ya Sh1 milioni na kati ya wadhamini hao mmjoa awe na mali isiyohamishika.

No comments: