Advertisements

Thursday, September 1, 2016

MADALALI WA NHC WATOA VITU NJE KATIKA OFISI YA GAZETI LA TANZANIA DAIMA LINALOMILIKIWA NA FREEMAN MBOWE

Madalali wa NHC wamefika katika ofisi za gazeti la  Tanzania Daima asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa ofisini kutokana na deni la pango la mmiliki wa gazeti hilo, Freeman Mbowe.

Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Neville Meena amesema wako kwenye msukusuko mkubwa lakini wanafanya jitihada za kukabiliana na hali hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unafanyika kama kawaida.


2 comments:

Anonymous said...

Ukiishi kwenye nyumba ya kioo usimtupie adui yako mawe! Hili halitaki shule kuelewa madhara yake!

Anonymous said...

Chaajabu huyu bwana mkubwa akataka watanzania tuamini kuwa "kwa yeye kulipa kodi ni jambo la kisiasa" jambo ambalo hata mkaanga chips wa mtaani anawajibika nalo.Labda ndio demokrasia anayoihitaji kwa wengine kulipa kodi ni halali kwake gharama za rent zina ingia kama net profit!