Advertisements

Thursday, September 15, 2016

MADEREVA WA TANZANIA WATEKWA NCHINI DRC

SERIKALI imesema imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo lililopo Jimbo la Kivu ya Kusini nchini Kongo DRC jana na jitihada za kuwaokoa madereva hao zinafanywa kupitia nchi zote mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriakiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga amesema malori hayo yanamilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji na mfanyabiasha wa Kenya.

Mindi amesema taarifa zilizopatikana zinasema watekaji ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambapo baada ya kuyateka magari hayo waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuyateketeza kwa moto malori manne ambayo yanamilikiwa na Dewji.

“Waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha dola za kimarekani 400 sawa na Sh milioni 8.7 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia,”amesema Mindi.

Amesema serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imechukua hatua za awali za kuwasiliana na serikali ya Kongo DRC. Tutawaletea ripoti zaidi.

No comments: