Advertisements

Sunday, September 18, 2016

MANISPAA YA KINONDONI YAVUNJWA RASMI, MEYA BONIFACE KAPOTEZA NAFASI YAKE

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kawaida.

Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.

“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.

Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.

Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.

3 comments:

Anonymous said...

MCHEZO KAMA HUO WALICHEZA SANA KULE ZANZIBAR KUGAWA MAJIMBO NA MAMBO MENGINE LAKINI HAIKUWASAIDIA KILA SIKU ZIKIENDA WATU WANAZIDI KUIKATAA CCM. NA HAPO DAR CHEZENI MNAVYOCHEZA LAKINI HAMTOKI

Anonymous said...

Siku zote hamfikirii maendeleo mnadhani kila jambo ni siasa.kwa mgawanyiko wa madiwani uliopo Dar it doesn't make any sense to think kuwa CCM wamecheza mchezo mchafu kwenye hili.ni wazi kuwa Kinondoni & Ubungo zote zitakuwa chini ya madiwani wa Ukawa.Pafike mahali tufocus kwenye issue za maendeleo na tuache hizi blabla za siasa.

Anonymous said...

Huu ni ujinga wa hali juu, kila kukicha ccm wanafikiria jinsi ya kuwadhibiti wapinzani, kwa nini hamkubali hali halisi kwamba mlishindwa kihalali kabisa mnataka mtawale kila kona kwa gharama yoyote, kama watu waliwakataa tafuteni sababu ni kwa nini siyo kulazimisha kutawala! Au laa badilisheni katiba tujue moja kwamba ni chama kimoja tuu kinatakiwa kitawale!
Ina-bore sana.