Advertisements

Monday, September 19, 2016

MH. MHAGAMA AKUTANA NA KAMATI YA URATIBU WA MAAFA MKOA WA KAGERA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifungua kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera Septemba 18, 2016, kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakiendelea na kikao cha kujadili na kufanya tathimini ya hali ya athari ya Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.Salum Kijuu akiwasilisha taarifa ya tathimini ya hali ya waathiri wa Maafa ya Tetemeko la Ardhi mkoani hapo wakati wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya Uratibu wa Maafa.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe.Deodatus Kinawiro akichangia hoja wakati wa Kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Kagera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: