Advertisements

Monday, September 19, 2016

MLIPUKO WAJERUHI WATU 29 KATIKA MJI WA MANHATTAN JIJINI NEW YORK

Mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu umetokea usiku wa jumapili huko Manhattan na kujeruhi watu 29.
Mtu aliyejeruhiwa akiwa kwenye machela yenye magurudumu akiwahishwa kupatiwa matibabu 

 Polisi Jijini New York wanachunguza kitu kingine kinachodhaniwa kuwa ni bomu la pili lililopo kwenye chombo cha kupikia maarufu kwa lugha ya kigeni kama pressure cooker.
 Picha za CCTV zenye kuogofya zinaonyesha mlipuko huo ukitokea New York katika eneo la jirani na Chelsea majira ya saa mbili na nusu usiku.


            Mmoja wa majeruhi akiwa amepatiwa huduma ya kwanza kwenye gari la wagonjwa

No comments: