ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 5, 2016

MHE. BALOZI WILSON MASILINGI AZIKAGUA TIMU ZA TANZANIA NA GHANA, DURHAM, NC KATIKA KUHITIMISHA ZIARA YAKE JIMBONI HUMO

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akipeana mkono na mmoja wa wachezaji wa Tanzania alipokagua timu hiyo  katika kuhitimisha ziara aliyofanya Durham na Winston Salem jimbo la North Carolina kwa kufanya mazungumzo na Mayor wa Durham, Mayor William"Bill Bell", kutembelea Mount Eagle College & University  na kuzungumza na Watanzania wa huko. katika mechi hiyo iliyochezwa siku ya Jumapili Septemba 4, 2016 Ghana iliibuka mshindi wa bao 3-1.

 Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Wilson Masilingi akiwa katika picha ya pamoja na manahodha wa timu zote mbili, mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Watanzania North Carolina, Bi, Gloria Alex (wapili toka kushoto) na Afisa Ubalozi Bwn, Abbas Missana (watano toka kushoto)
Picha ya pamoja.

mpambano ukiendelea.

Sean akilalama baada ya kukwatuliwa ndani ya 18 na refa kupeta.

Gloria Alex, mwenyekiti wa umoja wa Watanzania North Carolina akiongea na timu zote mbili baada ya mchezo kumalizika na kuwashukuru kwa mchezo mzuri ulioonyesha urafiki.

Mtoto Jonathan "kocha mtoto" wa timu ya Tanzania (kaptula nyekundu) akisikitika kwa mama yake baada ya Sean kukosa goli la wazi baada ya kipa wa Ghana kuutema mpira mguuni na yeye kupaisha mpira huo.

Mtoto Jonathan "kocha mtoto" wa timu ya Tanzania akigalagala chini baada ya Sean kukosa penati.
 Wakina shemeji wakifuatilia mpambano wakiwa na watoto wao.
Mashabiki wakifuatilia mchezo

 Goli la pili la Ghana.

 mashabiki
 Mashabiki wakifuatilia mpira

No comments: