Advertisements

Thursday, September 22, 2016

MIKUTANO YA NDANI YA VYAMA VYA SIASA RUKSA

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya.

JESHI la Polisi nchini limeondoa katazo lake la mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kuanzia leo. Ambapo vyama hivyo vitaruhusiwa kufanya mikutano ya ndani.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.

Kamishna Mssanzya amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba.

Jeshi la Polisi limesema limeamua kuruhusu mikutano hiyo ya ndani baada ya kuridhishwa na mwenendo wa shughuli za kisiasa nchini.

No comments: