Advertisements

Saturday, September 10, 2016

MISA YA KISWAHILI NEW YORK KESHO JUMAPILI

Image result for 120 East 106 Street, New York, NY 10029.
Wakristu wapendwa,
Tumsifu Yesu Kristu.
Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi, wanapenda kuwatangazia ya kuwa,
Misa yetu ya kiswahili itafanyika Jumapili ijayo, tarehe 11 Mwezi Septemba, 2016, Saa 8:00 mchana (Sunday 11, September 2016 at 2 pm). Tungeomba wakristu wote watanzania na Afrika ya Mashariki wajiunge nasi katika Misa hii.
Tunawakaribisha watu wote wanaopenda kuhudhuria ibada ya Kiswahili.

Anwani yetu ni: Kanisa la Mt. Cecilia, 120 East 106 Street, New York, NY 10029. Between Lexington and Park Avenue.

Chukua Train # 6. Mpaka kituo cha 110 St. Halafu tembea ukirudi mpaka 106 St.

Ni matumaini yetu kwamba mtafika kwa wingi. Karibuni tumtukuze Muumba Wetu kwa lugha yetu ya Kiswahili.
Mbarikiwe. Kutoka kwa Padre Peter Mushi na Padre Godfrey Amobi


Karibuni

No comments: