Advertisements

Thursday, September 1, 2016

PICHA: KUPATWA KWA JUA RUJEWA MKOANI MBEYA LEO



Hii ndio hali halisi ya Rujewa mkoani Mbeya baada ya kupatwa kwa jua leo Septemba 01 mwaka 2016(Picha hizi ni kwa hisani ya Michuzi Blog)

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala, (Kulia), Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete (katikati) na Mkuuwa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, wakitumia miwani maalum kuona tukiola kupatwa kwa jua huko Mbarali mkoani Mbeya hivi sasa Septemba 1, 2016

Pascal akitazama kupatwa kwa jua
Jua limeanza kufunikwa taratibu likiashiria kuanza kupatwa . Hadi sasa takriban theruthi moja imeshafunikwa na watu wengi wanaendelea kutizama kwa kutumia miwani waliopatiwa huku wengine wakitumia vifaa vingine vyenye uwezo wa kuwawezesha kuona tukio hilo.
Miwani iliyoletwa imetolewa kwa waliokuwa wamejipanga katika makundi ya watu 30 lakini imeshindwa kutosheleza mahitaji. Viongozi mbalimbali wa mikoa ya Songwe na Mbeya wanaendelea kuwasili eneo hili sambamba na makundi ya shule mbalimbali.
Mbali na kushuhudia tukio hilo, wananchi wengi wanalalamika kuwa kuna vyombo vya habari vya kimataifa lakini Serikali imeshindwa kuweka hata bendera ya taifa kutofautisha eneo la Rujewa na maeneo mengine ulimwenguni wanakoshuhudia kupatwa kwa jua.




Viongozi wa serikali, wanahabari wa ndani na nje ya nchi na wananchi wameshawasili katika eneo linalotumika kushuhudia kupatwa kwa jua.

Eneo hili lililopo Rujewa, Mbarali ambalo hutumika zaidi katika kuchimba mawe na kupasua kokoto leo limefurika watu ambao wapo hapo si kwa ajili ya kununua bidhaa hiyo ya ujenzi bali kusubiri kushuhudia tukio hilo la aina yake duniani.
Walimu wakiongozana na wanafunzi wa shule kutoka Mkoa wa Mbeya na jirani wamewasili hapa kama sehemu ya kuwafundisha wanafunzi kivitendo.
Askari wanarandaranda kila kona kuhakikisha usalama unaimarishwa.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala aliyewasili pia katika eneo hili, amesema tukio hilo limefungua fursa kwa kila mtu Mbeya hasa Mbarali.
Amevishukuru vyombo vya habari kwa kuutangaza mkoa na amewaambia wananchi wajikusanye katika makundi ya watu 30 ili wapewe vifaa vya kutazama kupatwa kwa Jua Tanzania.
Makalla amewataka wananchi kuwa makini kuangalia tukio hilo akisisitiza "Huu siyo mwisho wa dunia."
Waendesha bodaboda na bajaji wanaendelea kuwaleta watu hapa Rujewa kushuhudia kupatwa kwa jua.

No comments: