Advertisements

Tuesday, September 13, 2016

SHUKURANI KUTOKA ICT


“African Products expo” Iliandaliwa na kikundi cha wajasiriamali kutoka Tanzania wanaoishi katika mkoa wa Maryland nchini Marekani kijulikanacho kwa jina la ICT (Investment Consortium of Tanzanians in USA). Lengo na Madhumuni ya maonyesho haya yalikuwa kutangaza bidhaa toka Afrika katika jamii zetu hapa Marekani na hatimaye kuweza kupata soko katika bara la Amerika . Onyesho hili lilikuwa na washiriki kutoka nchi mbalimbali na lilihudhuriwa na watanzania na wageni kutoka nchi zingine za Afrika na Marekani. Onyesho hili litakuwa likifanyika kila mwaka na kushirikisha wajasiriamali kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Unaweza kununua chai na Kahawa kutoka Tanzania katika maduka haya yafuatayo.
  • Savanna International Market Inc at 117 N Frederick Ave # 4, Gaithersburg, MD 20877
  • Bismillah Halal Meat Market at International Plaza and Bay Street, 1401 University Blvd E, Hyattsville, MD 20783
Tunapenda kuwashukuru wajasiriamali wote walioshiriki na wateja waliofika kununua bidhaa za kutoka Afrika. Mungu akipenda tutaonana mwakani. Kwa mahitaji yote ya bidhaa kutoka Tanzania wasiliana nasi kwenye 240-813-5563.Asanteni
ICT

No comments: