Advertisements

Thursday, September 15, 2016

TAARIFA YA TULIPOFIKIA: MAZISHI YA JOEL LUGENDO


Ndugu watanzania; kamati ya mazishi inapenda kuwapa taarifa ya maendeleo ya msiba wa mwenzetu Joel Lugendo.


Mwili wa marehemu kusafirishwa kwenda Tanzania Jumamosi hii Asubuhi .

Wasindikizaji wa Mwili ambao ni Dada wa Marehemu na Mpwa wa Marehemu nao pia wataondoka Jumamosi kwenda Tanzania . 

Mazishi ya mpendwa wetu yanategemewa kufanyika huko Tanga , Tanzania Mara tu Mwili utakapowasili huko Nyumbani.

Tunawaomba muelewe kuwa kamati ya kujitolea imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana bila kuchoka ili kuhakikisha Mwanzetu anakwendaa kupumzika haraka iwezekanavyo.

Kuna mambo kadhaa yaliyojitokeza ambayo yalisababisha Mwili na wasindikizaji kuchelewa kuondoka. Lakini kwa juhudi ya Kamati na Familia tumefanikiwa kuweka mambo yote sawa.

Kama tulivyowaahidi ni kwamba tutatoa ripoti kamili ya mapato na matumizi Mara tu mwili utakaposafirishwa.

Tunawashukuru nyote kwa michango yenu ya mali na mawazo iliyosaidia kuweza kumsafirisha na kumzika ndugu yetu Joel Lugendo.

Asanteni;
Iddi Sandaly
Mchungaji Mbata.
Kamati ya Mazishi.

No comments: