Kufuatia changamoto zilizojitokeza katika zoezi la ufungaji wa mashine za kielektroniki zinazojulikana kama Electronic Fuel Pump Printer (EFPP) kwenye Vituo vya kuuza mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa na kufuatia agizo la Serikali kuwa wamiliki wa vituo vyote wawe wamefunga mashine hizo ifikapo tarehe 30 Septemba 2016, Wizara ya Fedha na Mipango, Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na Chama cha Wamiliki na
Waendeshaji wa Vituo vya Kuuza Mafuta Nchini (TAPSOA) umekutana na kujadiliana changamoto zilizopo katika zoezi la ufungaji wa mashine za EFPP na kukubaliana yafuatayo;-
a)Serikali imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya kufunga mashine za EFPP, ili kutoa nafasi kwa TRA ikishirikiana na TAPSOA kutatua changamoto zilizopo kwa sasa.
b)Wamiliki wa vituo vya kuuza mafuta ambao hawajakamilisha ufungaji wa mashine za EFPP waendelee kutumia mashine za mkono (ETR) mpaka hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.
c)TRA inawakumbusha wamiliki wote wa vituo vya kuuza mafuta kuhakikisha kuwa wanatoa stakabadhi za kielektroniki kwa kila mauzo wanayofanya ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwemo adhabu kwa kukaidi agizo hili la kisheria.
“Pamoja Tunajenga Taifa Letu
No comments:
Post a Comment