Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba nchini, Amon Mpanju akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,Wahariri,Viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini na taasisi mbalimbali wakati wa siku ya utoaji wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Seashells jijini Dar es salaam leo.Warsha hiyo imelenga kufanya tathmini ya masuala ya haki za binadamu nchini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa utekelezaji wa haki za binadamu.Pamoja na mambo mengine Mpanju alisema serikali haiungi mkono ndoa za jinsia moja na kuwataka wadau kuungana kupiga vita ndoa hizo ambazo kwa mujibu wa sheria na tamaduni za kitanzania hazikubaliki.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania (Tanzania Human Rights Defenders Coalition- THRDC) Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza jambo kwa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa klabu za waandishiwa habari (press clubs) wa mikoa mbalimbali waliokutana kujadili changamoto wanazozipata pamoja na kujadili rasmu ya sheria mpya itakayopitishwa bungeni hivi karibuni.
Rais mstaafu wa Umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania, Kenneth Simbaya akiwaomba viongozi wa press club waliofika katika mkutano uliokuwa ukijadili mswada wa sheria mpya ya vyombo vya habari
Baadhi ya viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
No comments:
Post a Comment