Advertisements

Monday, September 19, 2016

UWANJA WA NDEGE NDULI WAPONA KUTEKETEA KWA MOTO


Moto mkubwa ulizuka katika uwanja wa ndege wa Nduli manispaa ya Iringa. Moto huo ulisababishwa na uchaomaji mashamba yaliyopo jirani na uwanja huo. Kikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao ungeweza kuteketeza vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na majengo. Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye alishirikiana na kikosi cha zimamoto kuzima moto huo alisema " lazima wananchi wajue kutenga mashamba yao kuzuia mioto kusambaa kuanzia sasa yoyote atakaye sababisha moto kutoka kwenye shamba lake atachukuliwa hatua kali za kisheria." Mkuu wa wilaya aliagiza manispaa itengeneze kutumia bullodozer barabara ya kuzuia moto kuzunguka uwanja. Moto huo ulianza majira ya saa 7 mchana na kusambaa hadi kwenye uwanja wa kuondokea ndege (Runway) pia kusogelea eneo la kuhifadhia mafuta ya ndege na vifaa vya kuongozea ndege. Ulidhibitiwa vizuri hadi kufikia saa 9.43 moto ulikuwa umezimwa.

No comments: