Advertisements

Friday, September 30, 2016

Washtakiwa kesi ya akaunti feki ya tetemeko wapata dhamana

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Bukoba. Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba imewaachia kwa dhamana washtakiwa watatu wa kesi ya kufungua akaunti feki ya tetemeko mkoani Kagera.

Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza, Amantius Msole ambaye alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, amekwama na kurudishwa rumande baada ya kukosa mdhamini wa kuaminika.

Wametakiwa wasalimishe hati za kusafiria, kuwa wadhamini wawili kila mmoja anasaini bondi ya Sh5 milioni na hawaruhusiwi kutoka nje ya mkoa wa Kagera. Kesi itatajwa Oktoba 13.

No comments: