Advertisements

Friday, September 30, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla afanya ziara katika Hospitali ya Mkoa wa Kigoma

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokelewa na madaktari waandamizi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, wakati wa kuwasili Hospitalini hapo kwa ziara ya kikazi mapema jana Septemba 29.2016.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka kwa msimamizi wa Maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Kigoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mashine za ndani ya Maabara hiyo ambapo nyingi amebaini kuwa hazitumiki kutokana na ubovu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk.Chawote juu ya kufanyia maboresho Maabara hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha Upasuaji cha Hospitali hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo ya maboresho
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma (Hawapo pichani) wakati wa kuhitimisha ziara yake hiyo.
Baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao na kupata maoni yao juu ya utendaji kazi Hospitali hapo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Rufaa ya Maweni ya Mkoa wa Kigoma na kujionea mambo mbalimbali.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri aliweza kubaini mapungufu kadhaa ambapo amewataka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatatua matatizo hayo haraka. Miongoni mwa matatizo hayo ni pamoja na kutokuwa na mfumo maalum wa kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ili kudhibiti mapato huku akiwataka ndani ya miezi mitatu wawe wameshakamilisha mfumo huo.

Mbali na hilo pia amewataka kuzingatia utunzaji wa vifaa vya Maabara ya Hospitali hiyo kwani licha ya kuwa na jingo zuri lakini bado hali ya utunzaji imekuwa ndogo na hata kusababisha vifaa vingine havifanyi kazi.

Kwa upande wa Chumba cha upasuaji (Theatre) amewaagiza kuhakikisha wanaondoa kasoro zote muhimu kwani Chumba hicho kimekosa sifa ya kuitwa Chumba cha Upasuaji cha Hospitali ya Mkoa wa Kigoma baada ya kushuhudia ufinyu wa jengo lenyewe, ukosefu wa vifaa na hali nzima ya sehemu ya utendeaji kazi.

Naibu Waziri wa Afya ametembelea Mkoa Kigoma katika ziara yake ya siku mbili, awali aliweza kutembelea Kituo cha Afya cha Uvinza kilichopo Wilaya ya Uvinza, pamoja na Hospitali ya Heri Mission iliyopo Wilayani Buhigwa Mkoani humo.

No comments: