Advertisements

Thursday, September 1, 2016

WIZARA YA AFYA KUFANYA UZINDUZI WA KONDOMU MPYA MKOANI MWANZA.

Baada ya juzi Agost 30,2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuzindua aina mpya ya Kondomu iitwayo Zana Kondomu mkoani Mbeya, Uzinduzi kama huo unatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza Septemba 05,mwaka huu.

Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni (pichani), jana alisema mkoa wa Mwanza unatarajia kupokea ugeni kutoka wizara hiyo ambao utajumuisha wataalamu mbalimbali wa afya watakaokuwa wakitoa semina na elimu kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari, wakielezea juu ya uzinduzi wa kondomu hiyo.

Alisema miongoni mwa dhumuni la kuzindua aina hiyo mpya ya Kondomu, ni kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukwimwi ambapo Wizara itakuwa ikigawa bure kondomu hizo zenye ubora kwa wananchi, kote nchini.
Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, Atley Kuni
Baadhi ya Wanahabari mkoani Mwanza, wakimsikiliza Afisa Habari Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza.

1 comment:

Anonymous said...

Hii ndio Tanzania. Tunazindua CONDOM MPYA. Toleo jipya! Badala ya kuzindua dawa mpya! Liashiria kwamba watu waendelee kufanya mambo kwa toleo jipya. Kuna uhakika gani watumiaji wanatumia ipasavyo wakati pombe zinanyweka 24 hrs! Elimu ta afya ni ndogo sana wizara ya afya amkeni. Naibu waziri kufungia Dr. Mwaka badala ya kukaa na timu kuona hawa waganga na wavumbuzinwa dawa za kiasili wanapataje na zinasaidiaje ili kuboresha aunkutafuta utaalam zaidi imekuwa kero badala ya kudaadisi!!