ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 1, 2016

ASKARI POLISI APATWA KIGUGUMIZI KUSIMAMIA SHERIA

 Askari Polisi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), akipiga picha gari lenye namba T 297 AQE baada ya dereva wa gari hilo kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kusimama kwenye reli katika makutano ya reli na barabara ya Nyerere eneo la Gold Star jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana leo gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Mnazi Mmoja lilielekea Tazara. 
 Askari huyo akizungumza na dereva wa gari hilo aliweke gari lake pembeni ili alipishwe faini.
Askari huyo akisalimiana na abiria aliyeshuka katika gari hilo badala ya dereva na baada ya hapo alimwachia bila ya kumchukulia sheria yoyote kama wanavyofanya kwa madereva wengine wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Na Dotto Mwaibale

ASKARI polisi anayedaiwa kuwa ni wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), alikumbwa na kigugumizi na kushindwa kumchukulia sheria dereva wa gari dogo aina ya Corrona lenye namba T 297 AQE baada ya dereva wa gari hilo kukiuka sheria ya usalama barabarani kwa kusimama kwenye reli katika makutano ya reli na Barabara ya Nyerere eneo la Gold Star jijini Dar es Salaam majira ya saa sita mchana leo gari hilo lilikuwa likitokea maeneo ya Mnazi Mmoja lilielekea Tazara. 

Awali askari huyo baada ya kubaini kosa lililofanywa na dereva  huyo alilipiga picha gari hilo likiwa katikati ya reli wakati magari mengine yakiwa katika foleni.

Baada ya kupiga picha hiyo alimfuata dereva wa gari hilo alimtaka dereva wa gari hilo aweke gari lake pembeni ili aandikiwe faini.

Lakini kabla dereva huyo hajaweka gari hilo pembeni abiria aliyekuwa amekaa siti ya mbele ya gari hilo alitelemka na kujitambulisha kwa askari huyo ambapo walianza kusalimiana na kumruhusu aondoke bila kuchukuliwa hatua yoyote kama wanavyofanya kwa madereva wengine.

Akizungumzia tukio hilo dereva wa daladala linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto na Mnazi mmoja alisema sheria ni msumeno hivyo hata anapobainika ndugu jamaa, au rafiki wa askari kafanya kosa anapaswa kuguswa na sheria zilizopo.

"Yule jamaa kama sio askari polisi basi anaweza kuwa mwanajeshi au usalama wa taifa ndio maana yule jamaa aligwaya kumchukulia hatua" alisema dereva huyo.

Dereva huyo alisema kama kosa hilo lingefanywa na dereva ambaye hafahamiki na askari huyo ni lazima angelipa faini kwani hiyo ni kawaida ya askari hao kumkomalia mtu hata akiomba kusamehewa.



No comments: