Viongozi wa halamshauri zote mbili wa kwanza kushoto ni Diwani wa kang'ata, Mkurugenzi wa wilaya ya Handeni Wiliam Makufwe, Mkuu wa wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe, Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Mh Sauda Mtondoo na Mkurugenzi wa wilaya ya kilindi wakisiwakiliza wataalamu wa ramani (hawapo pichani) walipokuwa wakitoa ufafanuzi kuhusiana na mgogoro huo wa mpaka.
Viongozi wa halmashauri zote mbili wakiwasikiliza wananchi wa kijiji cha Negelo.
Wataalamu wa ardhi kutoka halmashauri zote mbili Handeni na Kilindi wakitoa ufafanuzi wa mgogoro huo wa mpaka,kwa wananchi .
Viongozi
wa halamshauri ya wilaya ya Handeni na Kilindi wamefanya ziara ya
kwenda kutatua mgogoro wa mpaka wa kijiji cha Gole kilichopo wilayani
Handeni na Negelo kilichopo wilayani kilindi.
Ziara hiyo iliofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 8,2016,imefamyika kufuatia kijiji cha Gole kulalamika kuwa kuna muwekezaji anafanya shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji uliotengwa tangu 2011.
Wakuu wa wilaya ya Handeni na Kilindi sambamba na Wakurugenzi wa wilaya hizo walifika eneo la mgogoro huo wakishirikiana na wataalamu kutoka pande zote mbili,na kusoma ramani iliyotumika kutenganisha mipaka ya wilaya na vijiji.
Mgogoro ulimalizika baada ya wataalamu hao wa mambo ya ramani, kutoa umiliki halali wa eneo aliyopo muwekezaji kuwa ni ndani ya Kijiji cha Gole.Wataalamu hao walieleza kuwa Sheria,taratibu na kanuni zitafuatwa katika kumuondoa muwekezaji huyo katika eneo hilo la hifadhi ili aweze kufanya shughuli zake za kiuchumi katika eneo husika kulingana na mpango bora wa ardhi.
Aidha uongozi uliwataka wataalamu wa pande zote mbili kukaa ndani ya siku kumi kuanisha mipaka inayotenganisha vijiji vya wilaya ya Kilindi na Handeni ili kuondoa utata kwenye vijiji vingine vilivyo na utata.
Mkurugenzi mtendaji kutoka wilaya ya Handeni, Bwa. William Makufwe akifafanua jambo kwa wananchi.
Mkuu
wa wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe akifafanua jambo kwa wananchi,
Mh Gondwe aliwaeleza Wananchi hao kuwa dhamira kuu ni kuhakikisha kwamba
amani inatawala pande zote mbili na kuhakikisha shughuli za kimaendeleo
zinasonga mbele na kwamba hakuna mwanachi yeyote anayekatazwa kwenda
kijiji kingine kufanya shughuli za kiuchumi,kikubwa ni kufuata sheria,
taratibu na kanuni za mahali husika.
Wakuu
wa wilaya Mh. Godwin Gondwe na Mh. Sauda Mtondoo pamoja na wananchi
wakikagua na kujionea hali halisi ya eneo ambalo mpaka unapita, na eneo
ambalo mwekezaji amechimba bwawa la maji kwa ajili ya mifugo yake.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Godwin Gondwe akipeana mkono na Mkuu wa wilaya ya Kilindi , Mh. Sauda Mtondoo kuonesha ishara ya kupongezana kwa kuelewa alama za mipaka ya maeneo yao ya kiutawala.
No comments:
Post a Comment