Advertisements

Friday, October 7, 2016

JAJI MKUU WA AUSTRALIA KUSINI AFANYA ZIARA NCHINI

 Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akipokea zawadi  ya picha  kutoka kwa  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika halfla fupi iliyofanyika  leo  tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa maktaba wa   Mahakama  ya Rufani  ya Tanzania.
 Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kulia) akizungumza kuhusu ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya mafunzo, sheria na shughuli za kimahakama baina ya nchi hizo mbili. (Kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mkutano  huo ulifanyika leo tarehe  7.10.2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba  na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.

No comments: