Advertisements

Thursday, October 6, 2016

JUMUIYA YA WATANZANIA CALIFORNIA YAFANYA KWELI, YATOA TAARIFA KWA WANAJUMUIYA WAO NA MARAFIKI JUU YA MISAADA YA TCO

TANZANIA COMMUNITY ORGANIZATION 
OF NORTHEN CALIFORNIA (TCO) 
912 Bayview Ave, Oakland, CA 94610 


510.290.9708, 510.472.7672
Ndugu Watanzania na marafiki wa Northern California.

Mwaka huu tutakuwa na fundraising nyingine ambayo itaambatana na kusheherekea kumbukumbu ya sherehe zetu za uhuru hapo Dec 10 2016. Fundraising ya mwaka huu itakuwa ni kusaidia vifaa/kifaa kwa zahanati (clinic) mojawapo kutoka kijiji kimojawapo Tanzania. 
Lakini kabla ya yote ni vizuri tuwape taarifa kwa ufupi juu ya juhudi zenu mlizofanya mwaka jana za kuwezesha kuchangia msaada wa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Shughuli ilifanyika Dec 19 2015 katika mji wa Oakland - California. Katika mapato yaliyopatiakana basi Umoja wetu (TCO) uliweza kusaidia shule ya msingi ya Buhangija ambayo ni shule ya albinos inayosaidia kuwasomomesha watoto hawa katika mazingira ya amani baada ya matukio ya kukatwa viungo kuwa mengi miaka michache iliyopita.
TCO (Tanzania Community Organization) kupitia michango yenu iliweza kusaidia kiasi cha milioni 6, tisini na saba elfu (tsh 6,097,000). Kiasi hiki kilitumwa kupitia kwenye serikali ya wilaya kwa kushirikiana na uongozi wa shule ili kuhakikisha msaada uliwafikia walengwa.

Matumizi yake yalikuwa kama ifuatavyo. Wanafunzi waliweza kusaidiwa :

1.Mashuka 200 kwa gharama ya tsh milioni mbili (2,000,000 tsh)

2. Kofia kubwa (kwa ajili ya jua) na tshirts 200 kwa gharama ya milioni moja

No comments: