Advertisements

Saturday, October 29, 2016

KAGERA SUGAR YASHINDWA KUTAMBA KWENYE UWANJA WAO WA NYUMBANI

Wachezaji wa Azam Fc wakimpongeza Nahodha wao John Bocco dakika ya 86 baada ya kuwapachikia bao la ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom VPL leo kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini. Bao hilo limeiwezesha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam kuibuka na pointi  tatu muhimu  baada ya kuinyuka Kagera Sugar mabao 3-2 katika mchezo ulifanyika leo Mkoani Kagera.
Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Azam FC, ulioifanya Timu hiyo ya Jijini Dar es Salaam kupanda juu  nafasi mbili kwenye msimamo baada ya kufikisha jumla ya pointi 19 katika mechi 12 za Ligi ilizocheza. 

Mshambuliaji Themi Felix, alianza kuishtukiza Azam FC kwa kuifungia bao la uongozi Kagera Sugar dakika ya 32 kabla ya Mudathir Yahya kusawazisha kwa bao zuri la shuti akimalizia pasi ya kichwa aliyodondoshewa na Bocco kufuatia faulo iliyochongwa na Erasto Nyoni.



Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili Azam FC ilikianza kwa kasi kubwa ikitaka kupata bao la uongozi lakini mabeki wa Kagera Sugar walikuwa kizuizi kikubwa kwa washambuliaji wa mabingwa hao wakiokoa hatari zote. 
Mwamuzi wa mchezo wa leo, Mathew Akrama kutoka Mwanza, aliamuru penalti ipigwe langoni mwa Azam FC baada ya beki Aggrey Morris kumfanyia madhambi Ally Nasoro ndani ya eneo la hatari, na penalti hiyo ilifungwa na Felix. 

Baada ya bao hilo, mabadiliko ya wachezaji watatu yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Azam FC kwa nyakati tofauti ya kuwatoa Gonazo Ya Thomas, Gadiel Michael na Jean Mugiraneza na kuingia Shaaban Idd, Frank Domayo na Khamis Mcha, yaliongeza uhai kwa timu hiyo na kupelekea kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi huo. 
Alianza Domayo dakika ya 80 aliyefunga bao zuri kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira uliotemwa vibaya na mabeki wa Kagera Sugar kabla ya Bocco kufunga la ushindi dakika sita baadaye akifunga kwa kichwa safi kufuatia krosi iliyochongwa na Shaaban Idd. 
Bao hilo linamfanya Bocco kufikisha mabao matano kwenye msimu huu wa ligi akizidiwa mabao mawili na Shiza Kichuya wa Simba, anayeongoza kileleni kwa mabao saba.

Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba
Timu zilivyokuwa zinaingia Uwanjani
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar
Kikosi cha Azam Fc
Kikosi cha Azam Fc kilichoanza dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Uwanja wa Kaitaba


Kikosi cha Azam Fc leo kilikuwa:

Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/Khamis Mcha dk 79, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Jean Mugiraneza/Frank Domayo dk 70, Ramadhan Singano, Salum Abubakar, John Bocco (C), Mudathir Yahya, Gonazo Ya Thomas/ Shaaban Idd dk 62
Ushindi huu pia ni wa pili mfululizo baada ya Timu ya Kagera kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga kwa bao 6-2 na sasa Timu hiyo kupoteza pointi 3 mbele ya Azam Fc kwa bao 3-2. Kitendo kilichowafanya Mashabiki wa Kagera Sugar kuandamana wakionesha Mabango katika Mchezo huo.
Mashabiki wakiwa na Jazba kubwa Uwanjani Kaitaba
Mashabiki wa Kagera Sugar wakiwa na Mabango wakionesha ujumbe wao kwa Timu yao inayoongozwa na Maxime.
Wakidai kuwa ana Tabia ya kuuza Mechi.Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakijiuliza
Kagera Sugar wakiwa hoi baada ya Azam Fc kusawazisha bao kwa kufanya 2-2
John Bocco ‘Adebayor’ akigombea mpira wa kichwa
Kichapo cha pili mfululizo
Waamuzi wa Mtanange huo
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa na Ujumbe wao
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar
Juu kwa juu Wanahabri wa Azam Fc wakichukua Picha
Bocco tena
Penati.... mpira ukipangwa

No comments: