Advertisements

Saturday, October 8, 2016

KIMBUNGA MATTHEW CHAENDELEA KULETA MADHARA MAKUBWA, ZAIDI YA MILIONI YA WAKAZI WA FLORIDA HAWANA UMEME

Hawa ni wakazi wa mji wa Mt. Augustine, Florida wakiwa wamezihama nyumba zao wakipata hifadhi ya muda kwenye shule ya Pedro Menendez wakifuata hali ya tahadhali iliyotangazwa kwenye majimbo hayo. Majimbo mengine yaliyotahadharishwa ni Georgia na Carolina ya kusini,
Kimbunga Matthew kikileta madhara jimbo la Florida na kuwaacha wakazi zaidi ya milioni moja bila umeme.
Mtu akitembea kwenye barabara iliyofurika maji mji wa Augustine, Florida.

Hapa ni ufukweni Daytona, Florida siku ya Ijumaa Oktoba 7, 2016 kimbunga Matthew kilipoleta madhara makubwa kwenye ufukwe huo, Kwenye picha ni mdau akipata picha za za mawimbi ya bahari ya Atlantic kwenye ufukwe wa Daytona, Florida.
Hotel ya Hilton mji wa Daytona ikiwa imeharibika baada ya kugongwa na kitu kizito kilichorushwa na upepo mkali wa kimbunga Matthew.
Daytona, Florida inavyoonekana siku ya Ijumaa Oktoba 7, 2016 baada ya kimbunga Matthew kuleta madhara makubwa.
huu sio mto ni barabara ikiwa imefurika maji  yaliyosababishwa na kimbuga Matthew katika mji wa Mt. Augustine, Florida siku ya Ijumaa Oktoba, 2016.

Ufukwe wa Cocoa, Florida ukipata mawimbi mazito kutokana na Kimbunga Matthew.
Wadau wakitakiwa kutoka Disney World kwa kulinda usalama wao na hii itakua na mara ya tatu katika historia Disney World kufungwa baada ya kufunguliwa mwaka 1971. Ilifungwa mara mbili kwa ajili ya madhara ya vimbunga na mara nyingine ilifungwa nusu siku baada ya mashambulio la Septemba 11, 2001 Picha kwa hisani ya The Huffington Post na Market Watch

No comments: