Advertisements

Saturday, October 15, 2016

Mama wa Mitindo Asya Idarous Khamsini kunogesha Usiku wa Mashujaa Houston Texas

Asya Idarous Khamisin
Mama wa Mitindo Mkongwe anayefanya vizuri ndani ya Tanzania na Nchini Marekani, Asua Idarous Khamsini jumamosi hii ya Oktoba 15 anatarajia kunogesha usiku maalum wa Mashujaa Houston Texas, Nchini Marekani.

Katika shoo hiyo maalum ambayo imeandaliwa na Wakenya waishio Nchini humo, kiingilio ni Dola 40 za Kimarekani ( 40$) Kabla ya Jumamosi na mlangoni ni Dola 60 (60$).

Katika shoo Samba Mapangalla anatarajiwa kutumbuiza pia kutakuwapo wasanii wengine wakiwemo The Amani Band, Simple Simon huku mshehereshaji akiwa ni MC JT.

Shoo hiyo itafanyika katika ukumbi wa RIM JHIM HALL.

No comments: