Advertisements

Friday, October 7, 2016

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia njia za mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

 Mjumbe  kutoka  Jeshi la Polisi,Kamishna  Albert Nyamhanga akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya  Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo  yalifanyika jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto),  baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

No comments: