Advertisements

Friday, October 7, 2016

ZIARA YA JAJI MKUU WA AUSTRALIA YA KUSINI NCHINI TANZANIA

Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto) akisoma kitabu kinachohusu Chama cha Majaji Wanawake Tanzania wakati alipotembelea ofisini kwa Mwenyeji wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman.
Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akizungumza jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika ofisi ya Jaji Mkuu wa Tanzania, iliyopo kwenye jengo la Mahakama ya Rufani Tanzania, jijini Dar es Salaam. Mhe. Jaji Kourakis yupo nchini kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kujenga ushirikiano katika utendaji kazi wa Mahakama baina ya nchi hizo mbili. Kushoto ni Bi. Emma Gorman, Katibu wa Jaji Mkuu wa Australia Kusini.

No comments: