Advertisements

Wednesday, October 5, 2016

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA ENEO LILILOTENGWA KUJENGWA OFISI ZA ZIMAMOTO UWANJA WA NDEGE.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu,pia Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar Nd,Juma Saleh (katikati) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,pia Kaimu Waziri wa Mawasiliano na Usafirishaji Mhe, Haji Omar Kheir(kushoto)  jana alipotembelea Kituo cha Idara ya Zimamoto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiwa katika ziara maalum pamoja na kuangalia  eneo lililotengwa kujengwa Ofisi ya Ziama Moto katika Uwanja huo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi mbali mbali wakati alipotembelea eneo lililotengwa kujengwa Ofisi ya Ziama Moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana, akiwa katika ziara maalum ambapo   ametoa agizo la   miezi miwili kumalizika kwa ujenzi wa Ofisi za Zimamoto kwa Uongozi wa Idara hiyo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto)  akipata maelezo kutoka kwa Kamishana wa Idara ya Zima Moto Zanzibar Ali Abdalla Malimosi(katikati) wakati alipotembelea eneo lililotengwa kujengwa Ofisi ya Ziama Moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume jana.
[Picha na Ikulu.]05/10/2016. 

No comments: