Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella, akizungumza kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa Robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita, unaofanyika leo kwenye ukumbi wa jengo la NSSF Jijini Mwanza.
Jaji Mfawidhi Kanda ya Ziwa, Mhe.Robert Makaramba, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, akizungumza na wanahabari nje ya mkutano huo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi mkoani Mwanza, Mhe.Wilbert Martin Chuma, akizungumza kwenye mkutano wa robo Mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu mikoa ya Mwanza na Geita, unaofanyika leo Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF mkoani Mwanza, wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkuatno huo
Katibu wa JMAT ambaye pia ni Hakimu Mkazi mkoani Mwanza, Bittony Mwakisu (kulia) akiwa pamoja na Domician Mlashani, Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilayani Sengerema na mjumbe wa Kamati tendaji JMAT (kushoto).
Picha ya pamoja
Viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
Mongella amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili kwa uwazi masuala ya maadili kwa watumishi wa umma na kwamba yawe ajenda ya kudumu katika ngazi mbalimbali za utendaji serikalini hususani katika ngazi ya mahakama.
Amesisitiza mkutano huo kutoka na maadhimio yanayohimiza mahakama kutenda haki na kuleta manufaa kwa wananchi na kuondokana na malalamiko kwamba mahakama hazitendi haki katika maamuzi yake.
Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, chama hicho kinahakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kutenda haki na kuwafanya wananchi kutambua umuhimu wa chombo hicho katika utoaji wa haki.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma.
No comments:
Post a Comment