ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, October 8, 2016

SIJUI KAMA HII NI KWELI, JARIBU KUIPITIA NA WEWE

Image result for barrick gold mine
Mtandao wa gazeti la habari wa Toronto, Canada wa www.theglobeandmail.com tarehe 22-09-2016, uliandika habari kwamba... "POLICE KILLED 65, INJURED 270 at BARRICK MINE IN TANZANIA, INQUIRY HEARS"

katika undani wa habari hiyo unaeleza kwamba, Polisi Tanzania imefanya mauaji ya watu 65 na kujeruhi watu 270 kwa kipindi chote cha mgongano/migogoro kati ya wanavijiji wa vijiji jirani na askari hao wanaolinda mgodi huo unaomilikiwa na wawekezaji kutoka Canada..

Watu 270 (waliokufa) + watu 65 (waliojeruhiwa) ninsaqa na wastani wa mtu 1 kila siku kwa mwaka, ambaye anakutana na shambulio kutoka kwa walinzi wa mgodi huo.., inasikitisha sana, kuona idadi ya majeruhi ni ndogo kuliko watu waliopoteza maisha!

Watu wako kimya, nchi iko kimya, wanaharakati wako kimya, wanasiasa wako kimya, mashirika ya haki za binadamu na asasi za kiraia ziko kimya.., watu wanakufa hadi wacanada ndiyo wanaaandika habari hizi...

Tuendelee....

Kanuni za UN zinaoongoza biashara na haki za binadamu, kanuni ya 13, (The UN Guiding Principles on Business and Human Rights, principle 13) ambayo Barrick/Accacia waliiridhia inatoa onyo kwa kampuni ya kibiashara ambayo itajiingiza kwenye tabia mbaya ya uvunjifu wa haki za binadamu kutokana na shughuli zao za kila siku au matokeo ya mahusiano ya kibiashara na washirika wengine,

kwa kiingereza inasema; 'involved with adverse human rights impacts either through their own activities or as a result of their business relationships with other parties..

Barrick ambao wanamiliki 64% ya hisa za Accacia, waliwahi kukaririwa wakisema kwamba, 'wataendelea kutoa ushirikiano kwa Accacia katika juhudi zao za kuimarisha ulinzi na usalama katika mgodi wa North Mara'..

Sioni Mkurugenzi mtendaji wa ACACIA/BARRICK plc, Mr. Jean Vavrek, sioni kama akiitekeleza sera yake inayosema "... our respect for diversity and the transparent and ethical business environment"...

.., niwatake wamiliki, watendaji na wahariri wa magazeti ya kiintelejensia nchini kuacha kuandika habari mpasuko kuhusu 'walimu huko Mbeya' sasa waanze kuandika habari za kiuchunguzi kama hizi, (ambazo zinaandikwa na magazeti ya nje ya nchi, huku magazeti ya kwetu yakipambana na ProPESA.

Unaweza kuisoma hiyo habari katika link hii...
http://www.theglobeandmail.com/report-on-business/international-business/african-and-mideast-business/police-killed-65-injured-270-at-tanzanian-mine-inquiry-hears/article32013998/?service=mobile

Ukimaliza kuisoma, hebu sasa tumtake waziri wa nishati na madini, awatake hawa Accacia /Barrick wakanushe au wathibitishe habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la Toronto, Canada..., wakishindwa basi tumtake Rais wetu mpendwa, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli awasiliane na waziri mkuu kijana kabisa wa Canada, Justin Trudeau ili hawa jamaa ikiwezekana wachukuliwe hatua za kisheria!

Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida,
Kunta Kinte II

No comments: