Advertisements

Friday, October 7, 2016

TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU KUFANYIKA KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

Jumapili Oktoba 09, 2016 katika Kanisa la "EAGT Lumala Mpya International Church" Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, linatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amewahisi watu wote kufika kwenye tamasha hilo kwani kwenye kusifu na kuabudu, ana uhakika wa kuisikia sauti ya Mungu na huwa huru na kujitenga na dhambi ikizingatiwa kwamba kuna nguvu ya Mungu kwenye kusifu na kuabudu.


Mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana, Max Kemmy, amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kwamba litaanza kuanzia majira ya saa nane kamili mchana likiwa na ujumbe usemao, "Njoo Tuabudu Pamoja".
Na BMG

No comments: