Miss Tanzania 2016, Diana Edward (katikati) akiwa na mshindi wa pili, Grace Malikita na wa tatu, Maria Peter
MWANZA: Usiku wa Jumamosi, Oktoba 29, 2016 mrembo wa Kinondoni, Diana Edward Loy alitwaa taji la Miss Tanzania 2016 katika fainali zilizofanyika jijini Mwanza.
Hata hivyo pamoja na ushindi huo, haikuchukua muda akaanza kuubeba mzigo wa umaarufu kwa kusambaa taarifa zinazohusiana na umri wake.
Taarifa iliyosambaa ilisema:
MISS TANZANIA 2016
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
Ingawa sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi wakiwa na miaka miwili.
TAARIFA YA KUKANUSHA UVUMI HUO
Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;
1. Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.
2. Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.
3. Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda akaahirisha mwaka wake wa masomo.
4. Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya “Character assassination” lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.
TAARIFA JUU YA UVUMI KWA MISS TANZANIA 2016
Nachukua fursa hii kwanza Kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai na kuniwezesha kushiriki katika mashindano haya, kuishukuru Kamati ya Maandalizi ya Mashindano yaiss Miss Tanzania na pia kuwashukuru wapenzi na mashabiki wa masuala ya urembo, hususan wakazi wa jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi, na pia kuwashukuru wote waliyosafiri kutoka sehemu mbalimbali nakuja mpaka Mwanza kuja kushuhudia fainali za Miss Tanzania 2016 ambazo kwa mara ya kwanza zilifanyika jijini hapa mnamo tarehe 29.10.2016 nakuandika historia katika mashindano hayo.
Baada ya kusema hayo machache nataka kutoa ufafanuzi katika mambo mengi yaliyozungumzwa na kuwaacha wengi na sintofahamu:-
JINA KAMILI:
Diana Edward Loi Lukumay
KABILA: Mmasai
UMRI: Miaka 18, tarehe ya kuzaliwa, (01.06.1998) katika Hospitali ya Mount Meru Arusha.
Ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto wanne.
ELIMU: Shule ya Msingi ya Serikali ya Levolosi Mwaka 2005-2011
Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Serikali Arusha (Arusha Day Sec School) Mwaka 2012-2015.
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne ni daraja la pili (divsion two)
Alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano mchepuo wa Sanaa kwenda shule ya Wasichana ya Bwiru iliyopo jijini Mwanza, lakini kwa kuwa alikuwa tayari katika tasnia hii ya urembo aliamua kuto jiunga na masomo hayo kwakuwa tayari yalikuwa yameingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya vitongoji,ambapo nilijiunga na Kambi ya Miss Ubungo 2016/2017 ambapo alishika nafasi ya tatu.
Baada ya kuahirisha masomo ya kidato cha tano aliomba kujiunga na masomo ngazi ya cheti kozi ya maswala ya kodi katika Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) ambapo mpaka masomo yanaanza mwanzoni mwa mwezi wa oktoba tayari alikuwa kwenye kambi ya Miss Tanzania
Tumuunge mkono mlimbwende wetu ili atuletee Taji la Dunia.
Ahsanteni.
Charles William
Kaimu Ofisa Habari wake.
0716719589 (wilflow101@gmail.com). CnP
No comments:
Post a Comment