Advertisements

Saturday, October 8, 2016

‘USIKATE TAMAA’ YAWAFIKIA WAKAZI WA DAR


Wakazi wa Dar es Salaam wakiwemo wanafunzi waliokuwa katika kituo cha mabasi. wakipokea maji yaliyotolewa na kitengo cha Masoko cha MeTL Group katika kampeni hiyo.(Picha zote na Modewjiblog)
Ikiwa ni muendelezo wa kuisapoti jamii ya Tanzania katika jitihada za kupambana na umaskini, ujinga na magonjwa ambayo ni vikwazo vikubwa vya kimaendeleo nchini, kampeni ya USIKATE TAMAA imewafikia wakazi wa Dar es salaam.

Katika kampeni hiyo wananchi wamepatiwa elimu juu ya maji safi na taka.

Elimu hiyo imelenga kuwaelimisha juu ya magonjwa yanayosababishwa na maji taka kama kipindupindu, kuhara damu, homa ya tumbo pamoja na magonjwa ya ngozi.


Katika kampeni hiyo imesisitizwa haja ya kuwa makini wakati wanapotumia maji, kwani sio kila tone la maji wanalotumia ni safi na salama kwa matumizi.
Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Bi Fatema Dewji-Jaffer akiambatana na mtaalamu wa afya kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wamekuwa na kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii.


Amesema wamebaini kwamba kuna uhitaji mkubwa wa kutoa elimu kwa wanajamii juu ya afya zao kwani wengi wamekua wakitumia maji ambayo yanatoka katika chemchem au visima vilivyo kandokando ya mifereji ya maji taka na kemikali za viwandani.

Bi. Fatema amewataka wananchi katika uhamasishaji huo kutumia fursa zilizopo kutumia maji salama.

Kampeni ya maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu ni moja kati ya matukio ya mwendelezo wa kampeni ya “USIKATE TAMAA” yenye lengo la kusaidia jamii ya Tanzania katika mambo mbalimbali ikiwa kujifunza juu ya kulinda afya zao kwani maji ni kitu muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu na wakati huo huo ni chanzo kikubwa cha magonjwa hatarishi.

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipokea vipeperushi vyenye maelezo jinsi ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na maji.

Aidha katika kampeni hiyo amewahakikishia wananchi kuwa bidhaa za chapa ya MO inajitofautisha na chapa zingine kwani haijalenga katika kuuza bidhaa zake pekee bali na kusaidia jamii kuondokana na umasikini kwa kuhamasisha juu ya masuala ya kimaendeleo kwa kuzingatia afya.

Katika siku za karibuni ambapo Mkurugenzi huyo alipata nafasi ya kuzitembelea shule mbalimbali zilizoko jijini Dar es salaam na kutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kutoa misaada ya madaftari na kalamu kama sehemu ya kuonesha mfano kwa jamii katika kuleta maendeleo katika sekta ya elimu, alisema kampeni ya 'Usikate Tamaa' inataka kuamsha ari ya matumaini na kusonga mbele.

Aidha alisema Kampeni ya usikate tamaa haitaishia katika kutoa elimu tu bali kusaidia wananchi wake na kwa kuheshimu hisia zao, watakapokuwa wanakutana na bidhaa zenye chapa MO watambue ni kwa ajili yao zipo salama na zinawasaidia wao kukua katika kuwajibika kwenye maendeleo ya jamii bila ya kukata tamaa.
Burudani mbalimbali zikiendelea wakati gari la MeTL likipitia kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam na kutoa elimu ya maji safi na taka kupitia kampeni ya 'Usikate Tamaa'
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika mitaa mbalimbali wakigaiwa chupa za Maisha ya MeTL baada ya kupata elimu jinsi ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na maji.

No comments: