Advertisements

Thursday, October 27, 2016

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. (Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya.

No comments: