Alitoa wito kwa mshiriki atakayeshinda Tzshs. Milioni 30 za Maisha Plus aziwekeze katika uchumi wa viwanda. Grace PEMBA kutoka Mtwara aula Katika hatua nyingine, Waziri Mwijage ameahidi kumpatia mshiriki Grace Pemba kutoka Mtwara mashine ya kubangua korosho yenye thamani ya shilingi milioni nane. "Ukienda ripoti SIDO Mtwara, waambie Waziri amesema mnipe mashine ya kubangua korosho."
Grace aliyekua anafanya kazi katika saluni za kutengeneza nywele ameshauriwa kutumia mashine hiyo kujikwamua kiuchumi. Vipindi vya Maisha Plus vinarushwa na kituo cha Televisheni cha Azam Two na pia kupitia akaunti ya Youtube ya Maisha Plus. Taarifa zaidi kuhusu mashindano hayo zinapatikana katika tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv na kupitia mitandao ya Maisha Plus ya Facebook, Instagram na Twitter. Maisha Plus inaratibiwa na kampuni ya DMB na vipindi kutengenezwa na kampuni za True Vision Productions, KP Media na Pumzika Communications. #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTuGRACE Pemba kutoka MTWARA aula. Waziri Charles Mwijage amemuahidi kumpatia mashine yenye thamani ya shilingi milioni 8 ya kubangua korosho. Mhe. Mwijage ameyasema hayo wakati wa kuzindua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka iliyofanyika kijijini @maishaplus #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu A video posted by Masoud Kipanya (@masoudkipanya) on
No comments:
Post a Comment