Mabaki ya ndege iliyoanguka.
Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga selfie hizi.
Ndege iliyoanguka hii hapa.
Mmoja wa wachezaji wa klabu ya Chapecoense, Alan Ruschel (27) akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kutolewa kwenye ndege hiyo.
Alan Ruschel akipelekwa hospitali kwa matibabu.
Mabaki mengine ya ndege hiyo.
Mmoja wa majeruhi aliyenusurika kwenye ajali hiyo akipatiwa huduma ya kwanza.
Wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo.
NDEGE iliyokuwa imebeba watu 81, wafanyakazi tisa na abiria 72 ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin na kuua watu 76 huku watano pekee wakinusurika.
Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.
Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, ilianguka saa 4:15 jana usiku baada ya kupata hitilafu katika mfumo wake wa umeme na ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, huku akiongeza kwamba inawezekana kuna watu walionusurika.
Imeelezwa kuwa baada ya ajali ndege hiyo ilivunjika katika vipande viwili na kupelekea vifo vya watu 76 huku watano pekee wakinusurika wakiwemo wachezaji watatu wa Chapecoense ambao ni beki Alan Ruschel, makipa Danilo Padilha na Jacson Follmann pamoja na abiria wengine wawili Rafael Correa Gobbato na Ximena Suarez.
Baadhi ya picha zilizowekwa mitandaoni zinawaonyesha wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo.
No comments:
Post a Comment