Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote katika uchaguzi wa mwaka 2020.
Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,
“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule”alisema Mashinji.
Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.
Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.
2 comments:
Dr. Mashinji. Hebu piganieni swala la katiba kwanza na pia tukijua wazi kabisa Tume ya uchaguzi inafanya hila kubwa sana. Mnashindwa kuelewa kuwa walikuwa wameandaa matokeo kikamilifu kupitia IT yao na ndiyo.maana waliingilia kati.IT ya CDM. Tatizo ni Tume ya uchaguzi inayosimamiwa na mh. Lubuva imekaa vibaya mno na usishangae mkuu aakaipanga upya miwzi kadhaa kuelekea uchaguzi. Bila tume huru hata wakija wasimamizi toka dunia nzima bado watajishindisha. Jaribuni kufikiria tu ni kwa nini wafanyakazi wanahakikiwa kupitia vitambulissho NIDA na tume.
Pia kwa nini tume ya uchaguzi haifanyi zoezi la kuendelea kuwaandikisha wale waliokosa kijiandikisha kwenye daftari na wanaofikia miaka ya kuruhusiwa kupiga kura? Tume si ipo na wafanyakazi wapo? Wanafanya nini kwa sasa. Kama.mikutano imesimama hadi uchaguzi basi na tume ifunge kazi zake hadi uchaguzi.
Kuendelea kusema hatutakubali ni hadithi itakayonyima uhuru wa upinzani. Paazeni sauti zenu kutaka tume huru na katiba muafaka. Mbona mkuu ameweza kusaini sheria ya vyombo vya habari haraka bila kusita nini maana yake. Kuna sheria nyingi hazisainiwi kwa nini? Kuna maswali.mengi jiulizeni. Mjumbe wa halmashauri kuu ya CDM EL anayosema ndio mambo muhimu sana ya kuenddana na kasi ya awamu hii kwani haitaki kabisa kusikia ya wapinzani. Lazima kuja na mbimu na uwazi mbadala kuinhoa tume walau basi iwe na viongozi pande zote za upinzani na kuleta katiba mpya. 2020 sio mbali.
Ninaungana na mdau na wenye mapenzi mema. Kabisa lililo muhimu zaidi ni Tume huru ya uchaguzi na ikiendana na katiba ya nchi bila hivyo hakuna kutokubaliana ni yaleyale yataendelea miaka nenda. Fungukeni wana Upinzani kuna maonevu makubwa yanayozidi kuendelea na kusoma namba zilizofutika!!
Post a Comment